VIONGOZI WAKOSOA KUVURUGWA MIKUTANO YA RUTO.
Na Benson Aswani
Viongozi wa kisiasa nchini wanazidi kutoa hisia zao kutokana na kuvurugwa mikutano ya naibu rais William Ruto katika baadhi ya maeneo ambako amezuru nchini kisa cha hivi punde kikihusu eneo la Kondele kaunti ya Kisumu.
Wakiongozwa na Mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa viongozi hao wamekashifu vikali kitendo hicho wakisema kila mkenya ana Uhuru wa kuzuru na kufanya siasa maeneo yote nchini bila ya kuvamiwa au kudhulumiwa akisema wakenya ndio watakaochangua kiongozi wamatakaye kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2022.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na Mbunge wa Endebess Dkt Robert Pukose akikashifu vikali baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotumia vijana kuzua vurugu kwenye mikutano ya kisiasa, akitoa wito kwa wakenya kukumbatia siasa za amani.