VIONGOZI WAHIMIZWA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILI UTOVU WA USALAMA KERIO VALLEY.


Viongozi kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kukashifu utovu wa usalama ambao unashuhudiwa katika bonde la Kerio, kufuatia mauaji ya watu watatu siku ya ijumaa baada ya kupigwa risasi na washukiwa wa uvamizi katika eneo la Kaben eneo bunge la Marakwet mashariki kaunti ya Elgeyo marakwet.
Akizungumza baada ya kuhudhuria hafla ya kutawazwa shemasi wa kanisa la katoliki la Holy cross eneo la Kacheliba, seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amesema kuwa visa hivi vimekithiri katika siku za hivi karibuni na ni wakati hatua za dharura zinapasa kuchukuliwa.
Poghisio amesema kuwa viongozi wa pande zote mbili kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet wanapasa kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo hili, huku pia akiitaka serikali kutoegemea upande mmoja katika kuhakikisha usalama unadumishwa.