VIONGOZI WAHIMIZWA KUINGILIA KATI NA KUHAKIKISHA UKOSEFU WA MADAWA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI UNATATULIWA.


Wito umetolewa kwa idara ya afya kaunti hii ya Pokot magharibi kuhakikisha kuwa dawa za kutosha zinapatikana katika zahanati ya Otiot wadi ya Lomut ili kuwaepusha wakazi na changamoto ya kutafuta matibabu.
Uhaba wa madawa katika zahanati ya otiot wadi ya lomut umesababisha wakaazi wa eneo hilo kutembea mwendo mrefu kutafuta matibabu katika hospitali ya lomut jambo ambalo wanarai wizara ya afya katika kaunti hii kushughulikia kwa haraka.
Aidha wakazi hawa wanasema kuwa bara bara kutoka lomut hadi maros ni mbovu zaidi wakiitisha usaidizi kutoka kwa idara husika ili kushughulikia barabara hiyo kabla ya mvua kunyesha ili kuepuka hali ya barabara hiyo kuwa mbaya zaidi.
Wakati uo huo wamerai wizara ya elimu katika kaunti hii kuongezea shule ya maros walimu akisema kuwa walimu ni wachache mno katika shule huyo.