VIONGOZI WAHIMIZWA KUHESHIMU TUME YA UCHAGUZI YA IEBC BARINGO

Mwakilishi wa wadi ya bartabwa katika kaunti ya baringo reuben chepsongol amewarai viongozi wa muungano wa azimio la umoja kuheshimu tume huru ya uchaguzi na mipaka iebc na impe nafasi mwenyekiti wake wafula chebukati afanye kazi yake
Hii ni baada ya viongozi wa muungano huo kupinga uamuzi wa tume ya iebc ya kuendeleza kesi dhidi ya mwakilishi wa kike katika kaunti ya muranga sabina chege
Sabina, ambaye alikuwa akiwashawishi wafuasi wa kambi hiyo katika mkutano wa hadhara kaunti ya vihiga, alidokeza kuwa kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi wa mwaka 2017 na kwamba hali hiyo inaweza kutokea katika uchaguzi wa mwaka huu
Chepsongol ameongeza kuwa mwakilishi huyo anastahili kubeba msalaba wake