VIONGOZI WAHIMIZA AMANI KAINUK POKOT MAGHARIBI.


Viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kuhimiza wakazi wa eneo la Kainuk mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na Turkana kukumbatia amani na kujitenga na visa vya uvamizi ambavyo vimeshuhudiwa eneo hilo katika siku za hivi karibuni.
Wa hivi punde kutoa wito huo ni waziri wa kilimo na mifugo kaunti hii ya Pokot magharibi Geofrey Lipale ambaye amesema visa hivi vinarejesha nyuma juhudi za maendeleo akitoa wito kwa serikali kupitia vitengo vya usalama kuingilia kati na kuhakikisha hali ya utulivu inarejelewa.
Aidha amesema kuwa huenda shughuli ya kuwachanja mifugo eneo hilo ikakosa kutekelezwa kutokana na uvamizi ulioshuhudiwa eneo hilo juma jana.
Lipale ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kurejesha utulivu ili kurejelewa mipango ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa imepangiliwa kuendeshwa eneo hilo.