VIONGOZI WAENDELEA KUMWOMBOLEZA RAIS MUSTAAFU MWAI KIBAKI.


Viongozi mbali mbali nchini wameendelea kumwomboleza rais mustaafu Mwai Kibaki wakimtaja kuwa kiongozi ambaye alipelekea pakubwa kuimarika uchumi wa taifa hili katika utawala wake wa miaka 10.
Wa hivi punde kumwomboleza Kibaki ni seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Poghisio ambaye aidha amemtaja Kibaki kuwa kiongozi ambaye alijali amani ya taifa hasa baada yake kukubali kubuniwa serikali ya muungano hatua iliyomaliza ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Poghisio ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri katika serikali ya hayati Kibaki amesema ni katika utawala wake Kibaki ambapo mawasiliano yaliimarika nchini hasa kupitia mtandao ambao ulisambazwa maeneo mengi ya nchi hali iliyochangia maendeleo zaidi nchini.