VIONGOZI WAENDELEA KUKOSOA KUPANDISHWA BEI YA MAFUTA.


Viongozi mbali mbali nchini wameendelea kutoa hisia mseto kufuatia hatua ya mamlaka ya kudhibiti kawi EPRA kuongeza bei ya mafuta nchini.
Wa hivi punde kuzungumzia swala hilo ni mwakilishi wadi maalum kaunti hii ya Pokot magharibi Grace Rengei ambaye amesema kuwa hatua hiyo itawaathiri pakubwa wakenya wenye mapato ya chini ikizingatiwa bei za bidhaa za kimsingi pia zitapanda.
Rengei sasa ametoa wito kwa wabunge katika bunge la kitaifa kupitisha mswada wa kupinga nyongeza hiyo kutokana na hali kuwa wananchi hawakuhusishwa katika hatua hiyo.