VIONGOZI WAELEZEA WASIWASI WA KUSHUHUDIWA BAA LA NJAA POKOT MAGHARIBI.
Viongozi katika kaunti hii ya pokot magharibi wameendelea kutolea wito serikali kuu kuweka mikakati ya kuwasaidia wakazi wa kaunti hii ambao wataathirika na baa la njaa kutokana na ukame ambao umeshuhudiwa kwa kipindi kirefu mwaka huu.
Wa hivi punde kutoa wito huo ni seneta samwel poghisio ambaye amesema kuwa licha ya kuanza kushuhudiwa mvua katika kaunti hii, mimea ya wakulima wengi aliathiriwa na ukame ambao umekuwepo hali ambayo itapelekea mavuno duni mwaka huu.
Aidha poghisio ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la seneti ameilaumu serikali ya kaunti hii ya pokot magharibi kwa kile amedai kufuja fedha ambazo hutengewa hazina ya majanga, akidai kuwa fedha hizo zimekuwa zikitumika kando na malengo ambayo zimekusudiwa.