VIONGOZI WA UDA WAENDELEA KUKIPIGIA DEBE POKOT MAGHARIBI.


Viongozi wanaounga mkono chama cha UDA kinachohusishwa na naibu rais William Ruto katika kaunti hii ya pokot magharibi wameendelea kukipigia debe chama hicho.
Mbunge wa kapenguria Samwel Moroto ameelezea imani kuwa chama hicho kitatwaa viti vingi katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022 akidai kuwa kina umaarufu mkubwa miongoni mwa wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi.
Aidha Moroto amepuuzilia mbali mipango ya kubuniwa chama kipya katika kaunti hii akisema kuwa itakuwa vigumu kwa chama hicho kupata uugwaji mkono kutoka kwa wakazi na badala yake kuwataka viongozi zaidi kujiunga na chama cha UDA.
Aidha Moroto ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakazi wa maeneo ya mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ikiwemo Elgeyo marakwet na Baringo kudumisha amani na kujitenga na visa vya uvamizi wa mara kwa mara.