VIONGOZI WA SIASA WALAUMIWA KWA KUKITHIRI VIWANGO VYA CORONA NCHINI

Viongozi wa siasa ndio wa kulaumiwa kwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini.

Haya ni kwa mujibu wa viongozi wa kidini nchini ambao wamesema ni kinaya kwa serikali kufunga sehemu za ibaada ambazo zimekuwa zikitumika kuliombea taifa hali wanasiasa wamekuwa wakiandaa mikutano ya siasa bila kuzingatia kanuni za kukabili maambukizi ya virusi hivyo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa shirika la wachungaji nchini, church and clergy association of kenya kaunti ya Bungoma Hudson Ndeda viongozi hao wamemtaka rais uhuru kenyatta kutafakari upya kuhusu agizo lake kwani makanisa yamezingatia kikamilifu masharti hayo.