VIONGOZI WA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI KUAFIKA MAENDELEO.


Wito umetolewa kwa viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kuja pamoja na kushirikiana ili kuafikia maendeleo na kuimarisha uchumi wa kaunti hii.
Ni wito wake mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema kuwa miradi mingi ya maendeleo iliyoanzishwa katika kaunti hii imekwama huku mingine ikiendelea kuporomoka kutokana na ukosefu wa ushirikiano miongoni mwa viongozi.
Moroto amesema kuwa uchumi wa wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi utaimarika tu iwapo viongozi watashirikiana na kufufua miradi iliyoanzishwa akitaja kiwanda cha simiti na chuo kikuu cha kisii.
Wakati uo huo Moroto amekosoa mbinu ambayo inatumika na baadhi ya viongozi katika kaunti hii kubuni chama kipya akisema kuwa ni swala ambalo linapasa kuwahusisha viongozi wote pamoja na wakazi huku akisisitiza wito wake kwa wananchi kuunga mkono vyama vitakavyohakikisha kaunti hii inanufaika kwa miradi ya maendeleo.