VIONGOZI WA KISIASA POKOT MAGHARIBI WARUSHIANA CHECHE ZA MANENO


Siku moja tu baada ya gavana na wabunge wa kaunti hii kuzindua ukusanyaji wa saini za BBI katika uwanja wa maonyesho wa Kishaunet ambapo wanadaiwa kumkashifu kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Dkt. Samuel Poghisio kwa cheche za maneno, viongozi wanaomuunga mkono Poghisio wamejitokeza na kuwajibu viongozi hao vikali.
Wakimlenga mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing, wamemshutumu vikali mbunge huyo huku wakitaja matamshi yake kuwa ni utovu wa heshima kwa viongozi wengine.
Amutang’orok ni kiongozi wa wengi katika bunge la Pokot Magharibi.
Mwakilishi maalum Ozil Kasheusheu kwa upande wake amemsuta Lonyangapuo na wabunge wengine kwa kujilimbikizia usimamizi wa mchakato mzima wa BBI huku akisema chama cha KANU ndicho kilianzisha uhamasisho wa BBI katika gatuzi hili la Pokot.
Kasheusheu amepinga madai ya viongozi hao ya kutaka kujipiga kifua kwamba hao ndio walioshinikiza kubuniwa kwa eneobunge moja zaidi katika kaunti hii kulingana na pendekezo la bbi.
Amesema kiongozi wa wengi Samuel Poghisio pekee ndiye anafaa kupewa heko kwa kupigania ujio wa eneobunge hilo.Kuhusiana na suala hilo hilo la BBI, spika wa bunge la kaunti hii Catherine Mukenyang’ amewataka viongozi kutoweka siasa suala zima la BBI ambapo kila mmoja anataka kuonekana kwamba ndiye anayoiunga mkono kuliko mwengine.