VIONGOZI WA KIKE TRANS NZOIA WALALAMIKIA SHERIA DUNI ZA URIDHI.


Viongozi wa kike katika kaunti ya Trans nzoia wamelalamikia ongezeko la kesi zinazohusu uridhi wanazodai kuwa zinawakandamiza.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi mteule Sabina Wanjala, viongozi hao wameelezea kughadhabishwa na muda mrefu ambao unachukuliwa katika kesi hizo kabla ya kina mama waliofiwa na waume zao kupewa urithi wao kufuatia ukosefu wa sheria mwafaka ya kuangazia swala hilo.
Sabina sasa anapendekeza baadhi ya kesi zinazohusu urithi kusikilizwa nyumbani ili kuzuia gharama ambayo wengi wao hushindwa kumudu.