VIONGOZI WA KIDINI WASHAURI WANASIASA KUTOTUMIA HALI HII NGUMU KUJIPATIAUMAARUFU

KAKAMEGA
Viongozi wa dini ya Msambwa katika kaunti ndogo ya Lugari kaunti ya Kakamega wamewataka wanasiasa kutotumia hali ngumu inayosababishwa na ugonjwa wa Korona kujitafutia umaarufu kisiasa
Wakiongozwa na mzee Nasongo, James na Lwakaela wamesema serikali haifai kulaumiwa kwa hali ngumu ya uchumi inayoshuhudiwa nchini kwa sasa.

Aidha wazee hao wamewataka wananchi kutulia na kushirikiana na serikali ipasavyo katika mchakato mzima wa kumaliza maambukizi ya ugonjwa wa Korona

Viongozi hao wa dini ya Msambwa wamewataka wananchi kuendelea kumwomba Mungu na kuzingatia kanuni zilizowekwa na wizara ya afya kama vile kuvalia barakoa bila kusurutishwa na maafisa wa usalama ili kujilinda kutokana na janga la Korona.