VIONGOZI WA KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI WAMEHIMIZWA KUKOMA KUINGILIA MASWALA YA HOSPITALI

Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo amevunja kimya chake kufuatia shutuma ambazo zimeendelea kuelekezwa kwa serikali yake kutokana na hali inayotajwa kuwa mbaya katika hospitali ya Kapenguria.
Akizungumza na wanahabari Lonyangapuo ameelekeza lawama zake kwa bunge la kaunti kwa kile amedai kuwa ndio mhusika mkuu kwa masaibu ya wagonjwa katika hospitali hiyo kutokana kile ametaja kuwa kufunga bajeti ya kaunti.
Aidha Lonyangapuo ametetea huduma katika hospitali hiyo akisema licha ya changamoto zinazoshuhudiwa huduma zinazotolewa ni za kuridhisha na kuwa serikali yake imetenga kiasi fulani cha fedha kushughulikia hali katika hospitali hiyo.
Wakati uo huo Lonyangapuo amewasuta viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ambao wamelalamikia huduma katika hospitali ya Kapenguria akisema kuwa wanafanya hivyo kutokana na manufaa yao ya kisiasa akiwataka wanasiasa kutoingiza siasa katika maswala ya hospitali hiyo.