VIONGOZI WA DINI WATAKA MAKANISA KUFUNGULIWA BUNGOMA.


Viongozi wa dini katika kaunti ya Bungoma wameendelea kuishinikiza serikali kuruhusu kuendelea ibaada makanisani kwa kuzingatia kanuni za kukabili maambukizi ya virusi vya corona.
Viongozi hao wamesema kuwa kufunguliwa kwa makanisa kutawawezesha waumini kukutanika pamoja na kuliombea taifa wakati huu ambapo kunaendelea kushuhudiwa maambukizi zaidi ya virusi vya corona.
Wamesema kuwa maovu mengi yameendelea kushuhudiwa nchini ikiwemo watoto kutekwa nyara na kisha kupatikana wakiwa wameuliwa hali waumini wamenyimwa fursa ya kuombea maswala kama hayo.
Ikumbukwe kaunti ya Bungoma ni moja ya kaunti ambazo ziliwekewa masharti makali ya kukabili msambao zaidi wa virusi vya corona ikiwemo kufungwa maeneo ya kuabudu na kuongezwa masaa ya kafyu hadi kuanzia saa moja usiku hadi saa kumi alfajiri.