VIONGOZI WA DINI WAANZISHA MIKAKATI YA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUHUSU COVID-19.


Viongozi wa dini nchini wameanzisha mikakati ya kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuzingatia masharyti ya wizara ya afya katika kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Akizungumza katika warsha ya siku mbili ambayo imeandaliwa mjini kapenguria kaunti hii ya pokot magharibi, Dkt Godwin Mugo kutoka shirikisho la Christian health association of Kenya, amesema viongozi wa dini wanazuru kaunti mbali mbali kuhamasisha umma kuhakikisha masharti hayo yanazingatiwa.
Mugo amesema kuwa maambukizi ya virusi vya corona yameenea kutokana na hali kuwa wakazi wengi wamepuuza masharti ya wizara ya afya, hali ambayo imepelekea baadhi ya kaunti kuwekewa masharti zaidi.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwenyekiti wa wachungaji katika kaunti hii askofu Ronald Chumum, ambaye amewataka wananchi kutopuuza masharti hayo na badala yake kuyatilia maanani kwani watu wengi wamepoteza maisha kutokana na makali ya covid 19.