VIONGOZI WA DINI WAANDAA MAOMBI YA AMANI BARINGO.


Viongozi wa baraza la madhehebu mbali mbali kwenye kaunti ya baringo kwa ushirikiano na wale wa kisiasa katika eneo bunge la baringo kusini wameandaa mkutano wa pamoja kwa ajili ya kuombea amani na usalama katika eneo hilo.
Wakiongea kwenye mkutano huo ulioandaliwa katika eneo la marigat, viongozi hao wamesema kuwa ni kupitia maombi ndipo hali ya utulivu itarejea kwenye eneo hilo.
Viongozi hao hata hivyo wameshutumu uvamizi wa mara kwa mara ambao umekua ukishuhudiwa kwenye eneo bunge hilo hali ambayo imewapelekea wenyeji wengi kukimbia makwao.
Aidha viongozi hao wameitaka serikali kuanza kuwafidia waathiriwa wa uvamizi kutoka kwa wezi wa mifugo na pia gharamia mazishi ya watu wanaouwawa na majangili.