VIONGOZI WA DINI BUNGOMA WASHUTUMU VISA VYA UTEKAJI NYARA WA WATOTO.


Serikali imetakiwa kuchukua hatua za dharura na kukomesha visa vya utekaji nyara wa watoto na kisha kupatikana wakiwa wameuliwa.
Wakiongozwa na mwenyekiti askofu Samwel Manyonyi, muungano wa wahubiri wa alliance of ragistered churches mjini Webuye kaunti ya Bungoma, wametaka hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi ya washukiwa waliokiri kutekeleza mauaji hayo.
Aidha viongozi hao wamewataka wazazi kuwa waangalifu na wanao hasa wanapoeleka shule.
Wakati uo huo viongozi hao wa kidini wamewashutumu baadhi ya viongozi wa siasa kaunti hiyo kwa kutohakikisha usalama wa wanafunzi wanapoelekea shuleni akiwataka kuonyesha mfano bora kwa kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na wananchi