VIONGOZI TRANS NZOIA WATAKIWA KUWATAFUTA WAHISANI KUIMARISHA KAUNTI KIUCHUMI.


Viongozi katika kaunti ya Trans nzoia wametakiwa kuwatafuta wahisani kuwekeza katika sekta mbali mbali kaunti hiyo kama njia moja ya kupiga jeki kilimo na uchumi wa eneo hilo badala ya kutegemea fedha kutoka kwa serikali kuu pekee.
Akizungumza katika wadi ya Chepchoina mmoja wa viongozi eneo la Endebes Moses ainea amesema kuwa tayari amepata wahisani ambao watawekeza katika kiwanda cha maharagwe aina ya soya kwa wakulima wa eneo hilo akisema kuwa gunia moja la kilo 90 za maharagwe litanunuliwa kutoka kwa wakulima kwa shilingi alfu 12.
Aidha Ainea amesema kuwa kitakapomalizika kiwanda hicho na kuanza shughuli zake kitatoa zaidi ya nafasi laki moja za ajira kwa vijana katika kaunti hiyo ya Trans nzoia ili kupiga jeki uchumi wa wenyeji wa eneo hilo.