VIONGOZI TRANS NZOIA WATAKIWA KUHUBIRI AMANI KATIKA MIKUTANO YA SIASA.


Viongozi wa kidini katika kaunti ya Trns nzoia wametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuwa msitari wa mbele katika kuhubiri amani hasa wakati huu ambapo siasa za uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi agosti mwaka huu zimeshika kasi.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la makanisa katika kaunti hiyo ya Trans nzoia kasisi Aggrey Olumola viongozi hao wamesema kuwa hatua ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kunukuliwa wakitoa matamshi ya chuki ni tishio kubwa kwa amani ya wakenya.
Wakizungumza kwenye kanisa la church of God eneo la Mitume viungani mwa mji wa kitale katika ibaada ya jumapili, viongozi hao aidha wamewasihi wakenya kuwa makini wakati wa uchaguzi na kujitenga na viongozi ambao wanaeneza semi za chuki.