VIONGOZI TRANS NZOIA WATAKIWA KUELEWANA KUHUSU MIRADI ATAKAYOZINDUA RAIS.
Katibu mwandamizi katika wizara ya fedha Eric Wafukho amezuru Kaunti ya Trans-Nzoia Kutathmini miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kuu ikiwa ni pamoja na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kitale, Ujenzi wa barabara kuu ya Kitale-Suam na mradi wa maji wa Kiptogot- Kolongolo ambayo inatarajiwa kukamilika kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Kwenye mkao na wanahabari mjini Kitale Wafukho ametoa wito kwa viongozi Kaunti ya Trans Nzoia Kuketi pamoja na kuelewana kuhusu mapendekezo ya miradi ya maendeleo wanayotaka Rais Kenyatta kushughulikia anapopanga kuzuru Kaunti za Bonde la Ufa na zile za Magharibi mwa Kenya ikiwa ni paomaja na Kaunti ya Trans-Nzoia.
Wakati huo huo Wafukho ameelezea kuwa baadhi ya miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na serikali kuu imechukuwa muda mrefu kukamilika kutokana na changamoto za hali ya anga mbali na kucheleweshwa kwa malipo kwa wanakandarasi.