VIONGOZI TRANS NZOIA WASHUTUMU MARUFUKU YA UKULIMA KWENYE MISITU.


Viongozi Kaunti ya Trans-Nzoia wanaendelea kushutumu vikali Sera ya wizara ya misitu na wanyama pori kupiga marufuku ukuzaji wa chakula haswa zao la mahindi kwenye misitu maarufu shamba system wakisema kwamba marufuku hiyo haifai.
Wakiongozwa na mbunge wa Endebes Dkt Robert Pukose viongozi hao wamesema hatua hiyo huenda ikahujumu ajenda kuu ya serikali ya utoshelezaji wa chakula nchini, kwani jamii nyingi eneo hilo wanategemea misitu kwa ukuzaji wa chakula kwa familia zao na hata kukimu mahitaji yao ya kila siku.
Aidha Dkt Pukose sera hiyo inapaswa kutupiliwa mbali kwani tangu jadi wenyeji wamekuwa wakikuza mimea yao na kutunza miti, akisema sera hiyo huenda ikahujumu utunzaji wa mazingira haswa misitu nchini.