VIONGOZI TRANS NZOIA WASHUTUMU KUFURUSHWA MASKWATA KATIKA ARDHI YA ADC.


Viongozi kutoka Kaunti ya Trans Nzoia wameitaka serikali kupitia wizara ya kilimo kuangazia upya kufurushwa kwa maskwata katika ardhi moja inayodaiwa kumilikiwa na shirika la ustawishaji Kilimo nchini ADC.
Wakihutubu eneo bunge la Endebess viongozi hao wakiongozwa na Alwain Sasia wamesema wengi wa maskwata hao wamekuwa wakifanya kazi katika shirika hilo kwa miaka mingi ila kwa sasa wanaishi maisha ya uchochole baada ya kufurushwa.
Wakati huo huo Sasia ametoa wito kwa idara ya mazingira na misitu, kuwaruhusu wenyeji eneo hilo kuendelea kukuza mimea yao kwenye misitu akisema kuwa wengi wa wakaazi eneo hilo wanategemea kilimo kupata kipato chao cha kila siku.
Aidha Sasia amewahimiza wenyeji kuchukua vitambulisho na kujisajili kama wapiga kura iwapo wanataka kuleta mabadiliko ya uongozi eneo hil

[wp_radio_player]