VIONGOZI TRANS NZOIA WAPONGEZA HATUA YA KUPUNGUZWA BEI YA MBOLEA.
Viongozi mbalimbali Kaunti ya Trans Nzoia wanaedelea kupongeza hatua ya serikali kuu kupitia kwa wizara ya Kilimo kuwapunguzia wakulima bei ya pembejeo wakisema itasadia katika kupunguza gharama ya uzalishaji wa chakula nchini.
Wakiwahutubia wanahabari mjini Kitale wakiongozwa na Musoke Muliro mgombea kiti cha Useneta Kaunti ya Trans Nzoia kwa tiketi ya chama cha ODM, wametaka wizara ya kilimo kuhakiksha mbolea hiyo ya bei nafuu inawafikia wakulima mashinani ili kuwawezesha kukuza mimea yao licha ya changamoto ya mabadiliko ya hali ya anga huku msimu wa upanzi ukiendelea kuyoyoma.
Wakati uo huo Musoke ametoa wito kwa serikali kuu kushughulikia kwa haraka tatizo la uhaba wa mafuta nchini akisema hali hiyo pia inahujumu swala la kilimo kwani wakulima wengi wanatumia mafuta ya Diseli kwenye trekta zao katika matayarisho ya mashamba, akisisitiza haja ya serikali kuwaelezea wakenya chanzo kikuu cha ukosefu wa mafuta nchini.