VIONGOZI TRANS NZOIA WAPINGA MABADILIKO KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI.


Baadhi ya viongozi kutoka Kaunti ya Trans Nzoia wamepinga vikali hatua ya baadhi ya wabunge wa kitaifa kutaka kubadili sheria za usimamizi wa uchaguzi na kurejesha mfumo wa zamani wa kuhesabu na kutangaza kura za urais.
Wakiongozwa na Samuel Juma Kiboi viongozi hao wamesema hatua ya kubadili sheria hiyo huenda ikahujumu shughuli za usimamizi wa uchaguzi mkuu mwaka huu, akitaka Mwenyekiti wa IEBC Wafula chebukati kutokubali sheria hiyo mpya.
Wakati huo huo Kiboi ametaja kuwa kuwekezwa kwa mabilioni ya fedha za mtoza ushuru katika tecknolojia mpya ya utandawazi kisha kufutilia mbali ni Kinyume cha sheria na matumizi mabaya ya kodi ya mlipa ushuru.