VIONGOZI TRANS NZOIA WAONYWA DHIDI YA KUENDELEZA SIASA MAZISHINI.
Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Trans nzoia wametakiwa kukoma kupeleka maswala ya kisiasa katika hafla za mazishi.
Ni wito wake mshirikishi wa usalama eneo la bonde la ufa George Natembeya ambaye amesema kuwa viongozi wote wanastahili kutumia fursa hizo kuomboleza na waliofiwa pamoja na kuwapa msaada mahali panapostahili ila si kutumia kumbi hizo kuendeleza siasa.
Wakati uo huo Natembeya amewakemea wanasiasa ambao wametumia swala la chuo kikuu katika kaunti hiyo kuwa la kisiasa kila kunapokaribai uchaguzi mkuu akiwahakikishia wakazi kuwa serikali itaweka chuo kikuu katika moja ya mashamba ya kilimo ADC