VIONGOZI TRANS NZOIA WAKOSOA ADHABU FINYU INAYOTOLEWA KWA WABAKAJI.

Na Benson Aswani
Viongozi wa kike Trans nzoia wametaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wanaoendeleza visa vya ubakaji na utungwaji mimba wasichana eneo hilo wakilalamikia hatua ya kutolewa adhabu finyu kwao na mahakama.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ann wanjiku pamoja na lilian siyoi, viongozi hao wamelalamikia hatua ya mahakama kutoa adhabu ya chini kwa wahusika huku wakilalamikia ongezeko la visa hivyo.
Aidha wanataka kuanzishwa msako wa kuwanasa wahusika kuwalazimisha kufanyiwa vipimo vya DNA wawajibikie matendo yao.