VIONGOZI TRANS NZOIA WADAI KUINGIZWA SIASA KATIKA SHUGHULI YA KUTOA VITAMBULISHO.
Viongozi kutoka Endebess Kaunti ya Trans Nzoia wamelalamikia kile wametaja kuhangaishwa vijana wanaotaka kujisajili kupata vitambulisho vya kitaifa na maafisa husika .
Wakiongozwa na mbunge wa Endebess Dkt Robert Pukose viongozi hao wamesema vijana wamekuwa wakihangaishwa na wakuu wa utawala eneo hilo jambo ambalo limepelekea wengi wa vijana kukosa stakabadhi hiyo muhimu na kuchangia idadi ndogo zaidi ya vijana wanaojitokeza kupata stakabadhi hizo.
Aidha Dkt Pukose ameonya baadhi ya viongozi wa utawala kwa kujiingiza katika maswala ya kisiasa hivyo kuwapatia wakati ngumu vijana hao kijiandikisha kupata vitambulisho mbali na kuwa wapiga kura, akitaka maafisa husika kugatua zoezi hilo ili kuwafikia wenyeji wengi mashinani.