VIONGOZI TRANS NZOIA APINGA SHINIKIZO ZA KUMBANDUA AFISINI MWENYEKITI WA IEBC WAFULA CHEBUKATI.
Baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya Trans nzoia wanawakashifu wale wanaoshinikiza kutimuliwa kwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini IEBC Wafula Chebukati kwa kile wanadai wanaoshinikiza hilo wanataka kulemaza tume hiyo kwa masilahi yao ya kibinafsi
Wakiongozwa na mbunge wa kwanza Ferdnand Wanyonyi na mwakilishi wadi ya kapomboi Bernad Wanjala, wamesema tume hiyo inapaswa kupewa wakati mwafaka kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao baada ya makamishna wanne kuidhinishwa kujaza pengo lililowachwa.
Wanasema hatua ya kumtimua chebukati inanuia kuwafaa wachache.
Wakati uo huo mbunge huyo ametaka joto la kisiasa linaloshuhudiwa kwa sasa kupunguzwa kwa manufaa ya taifa hili akiwataka wanaogombea viti mbalimbali katika uchaguzi ujao kuuza sera zao kwa wapiga kura badala ya kutupiana cheche za maneno