VIONGOZI TIATI WAAPA KUSHIRIKIANA KATIKAKUMALIZA WIZI WA MIFUGO.
Viongozi eneo bunge la Tiati kaunti ya Baringo wameahidi kushirikiana na maafisa wa usalama pamoja na wakazi ili kuwakabili wezi wa mifugo wanaodaiwa kutoka eneo bunge hilo.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Tangulbei Shedrack Mailuk, viongozi hao wamesema kuwa watahakikisha wanohusika katika wizi wa mifugo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha Mailuk ameirai serikali kusitisha kabisa oparesheni ya kutwaa silaha haramu ambayo imekuwa ikiendelea eneo bunge hilo akisema imewaathiri wakazi wengi wasiokuwa na hatia.