VIONGOZI POKOT WAHIMIZWA KUWAKUMBUKA AKINA MAMA WALIOGOMBEA VITI TOFAUTI NA KUKOSA KUFAULU KWA KUWAPA UONGOZI KWA SERKALI ZA KAUNTI


Na Benson Aswani
viongozi wa kisiasa wa jinsia ya kike katika kaunti hii ya pokot magharibi wamelalamikia kutelekezwa pakubwa wanasiasa wa kike wanaogombea nyadhifa za kisiasa na kisha kukosa kufaulu katika nyadhifa hizo kwenye chaguzi za humu nchini.
Wakiongozwa na aliyekuwa mwakilishi wadi maalum Lucy Lotee, wanasiasa hao wamesema kuwa kinyume na ilivyo kwa wenzao wa kiume ambao huteuliwa katika nyadhifa mbali mbali na vyama vyao wanapofeli katika uchaguzi ,wanasiasa wanawake hupuuziliwa mbali na vyama hivyo.
Bi Lotee amesema kuwa wengi wa wanasiasa wanawake wanapitia wakati mgumu baada ya kupoteza katika uchaguzi hasa kutokana na hali kuwa wanatumia raslimali zao nyingi katika chaguzi hizo hali inayowaacha katika hyali ya umasikini.
Ametoa wito kwa viongozi hasa katika kaunti hii pamoja na vyama vya kisiasa kuwa na sera ambapo mwanasiasa wa kike anaposhindwa katika uchaguzi anapewa nafasi ya kujitafutia riziki kwani wengi wao wana tajriba ya kuhuduma katika nyadhifa mbali mbali.