VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WAUNGA MKONO MASHARTI MAPYA YALIYOTANGAZWA NA RAIS KENYATTA

Baadhi ya viongozi katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wametetea masharti mapya ambayo yalitangazwa na rais uhuru kenyatta katika kukabili maambukizi zaidi ya virusi vya corona.
Mbunge wa Sigor Peter Lochakapong amesema kuwa rais alilazimika kuchukua hatua hiyo ili kuwalinda wakenya dhidi ya maambukizi zaidi ya virusi hivyo hatari, akiwahimiza wakazi wa kaunti hii kufuata maagizo yaliyowekwa na wizara ya afya ili kusalia salama.
Hata hivyo Lochakapong ametoa wito kwa rais uhuru kenyatta kuzingatia watahiniwa wa kcse ambao wanafanyia mitihani hiyo katika sehemu zilizofungwa na si wenyeji wa kaunti hizo, ili wawezeshwe kurejea nyumbani pindi watakapokamilisha mitihani yao.