VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUUNGANA ILI KUAFIKIA MAENDELEO.
Wito umetolewa kwa viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kuja pamoja na kushirikiana ili kuafikia maendeleo na kuimarisha uchumi wa kaunti hii.
Ni wito wake mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema kuwa migawanyiko miongoni mwa viongozi imepelekea kaunti hii kusalia nyuma kimaendeleo hali inayofanya kutoheshimika ilikinganishwa na viongozi kutoka maeneo ambayo yameimarika kimaendeleo.
Moroto sasa anawataka viongozi katika kaunti hii kutowapotosha wakazi kwa kuwapeleka katika vyama ambavyo havitapelekea kuafikiwa lolote na badala yake kuhakikisha kuwa wanajiunga na vyama vitakavyowapelekea kuwa serikalini ili kunufaika na miradi ya maendeleo.