VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUTOTUMIA FEDHA ZA BASARI KABLA YA WATAHINIWA WA KCPE MWAKA 2021 KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA.


Wito umetolewa kwa viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kutopeana pesa za busary ila waziweke hadi wanafunzi watakapojiunga na kidato cha kwanza.
Akipongeza matokeo bora ambayo yamerekodiwa miongoni mwa shule za kaunti hii ya Pokot magharibi katika mtihani wa KCPE katibu wa chama cha walimu nchini KNUT tawi la Pokot magharibi Martine Sembelo amesema wapo wanafunzi wengi ambao walifanya vyema katika mtihani huo kutoka jamii masikini.
Sembelo amesema huenda fedha hizo zikatumika kabla ya wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la nane KCPE kutoka jamii masikini kujiunga na shule za upili hivyo kufeli kuendelea na masomo yao.
Wakati uo huo Sembelo amewashauri wazazi kutowakaripia wanao ambao hawakufanya vyema katika mtihani wa KCPE akisema kuwa kila mwanafunzi aliyefanya mtihani huo na kupokea matokeo ana nafasi katika shule za upili.