VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUONDOA SIASA KATIKA MIRADI YA SERIKALI.


Wito umetolewa kwa viongozi wa siasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kukoma kuingiza siasa katika miradi ya serikali kwenye taasisi za umma ikiwemo vituo vya afya pamoja na taasisi za elimu.
Ni wito wake gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ambaye amesema kuwa wengi wa viongozi wa kisiasa katika kaunti hii wameshindwa kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao ya uwakilishi na badala yake kupeleka siasa kwenye miradi ya serikali.
Wakati uo huo Lonyangapuo amesema kuwa huduma za afya katika kaunti hii ya Pokot magharibi sasa zitaimarika zaidi baada ya serikali kununua magari mawili ya ambulansi na ambayo yana vifaa vya kuwahudumiwa wagonjwa hata wanaposafirishwa.
Aidha gavana Lonyangapuo amesema chumba cha kuwahudumia wagonjwa mahututi ICU katika hospitali ya Kapenguria kimekamilika na kitafunguliwa rasmi hivi karibuni ili kuwapunguzia mzigo wagonjwa kusafirishwa hadi mjini Eldoret.