VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WATAKA KUONGEZWA MUDA WA MAZUNGUMZO YA AMANI BARINGO


Oparesheni ya kiusalama ikitarajiwa kurejelewa leo katika kaunti ya baringo, seneta wa kaunti hii Samwel Poghisio ameitaka serikali kuwapa muda zaidi viongozi wa kaunti hii ya Pokot magharibi na Baringo kwa mazungumzo na wakazi wa Tiati kabla ya kurejelewa oparesheni hiyo.
Poghisio amesema kuwa muda ambao serikali ilitoa kwa viongozi hao haujakamilika kwani ulifaa kukamilika tarehe 23 mwezi huu wa aprili, akiongeza kuwa hawakufahamishwa kuhusu hatua ya kurejelewa oparesheni hiyo.
Wakati uo huo Poghisio ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kujitenga na maswala ya uhalifu na badala yake kukumbatia amani ili kuafikiwa maenedeleo eneo hilo analosema lingali nyuma zaidi.