VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WASHUTUMIWA KWA KUENDELEZA UFISADI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO.


Viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wamelaumiwa kufuatia kazi duni ambayo inafanyika kwenye miradi mbali mbali inayotekelezwa katika kaunti hii.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki seneta wa kaunti hii samwel poghisio amewashutumu baadhi ya viongozi anaosema wanahusika katika kupora fedha zinazotengewa miradi hiyo hali inayowafanya wanakandarasi kutekeleza kazi duni.
Wakati uo huo poghisio amemshutumu mbunge wa pokot kusini David Pkosing kwa kile ametaja kuwa kutumia nafasi yake kama mwenyekiti wa kamati ya bunge la taifa kuhusu barabara kujipigia debe miongoni mwa wakazi.
Poghisio sasa ametoa wito kwa viongozi katika kaunti hii kuzingatia pakubwa kuwahudumia wananchi na kutoyajali maslahi yao ya binafsi hali inayowafanya kujilimbikizia fedha za umma huku wananchi wakihangaika kwa kutopata huduma bora.