VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WAMSIHI KINARA WA CHAMA CHA ODM KUREJEA TENA POKOT MAGHARIBI.


Ziara ya kinara wa chama cha ODM Raila Odinga katika kaunti hii ya Pokot magharibi imeendelea kuibua hisia mbali mbali miongoni mwa baadhi ya viongozi wa kisiasa kaunti hii.
Wakiongozwa na mgombea kiti cha ubunge eneo la Kacheliba John Lodinyo, viongozi hao wamesema kuwa ziara hiyo ilitekwa nyara na viongozi wa chama cha KUP ambao wameashiria kuungana na ODM, wakimtaka Raila kupanga upya ziara hiyo iwapo anataka uungwaji mkono kutoka kaunti hii.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mgombea ubunge eneo bunge la Pokot kusini Stephen Kolemuk ambaye amedai huenda juhudi za Raila kwa taifa hili zikadidimizwa na baadhi ya viongozi ambao huenda akashirikiana nao kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.