VIONGOZI POKOT MAGHARIBI WALAUMIWA KWA KUENDELEZA SIASA ZA MAPEMA.


Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Pokot magharibi Samwel Poghisio amewakosoa baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti hiyo kwa kile amesema kwamba wameanza kujihusisha na siasa za mapema miezi michache tu baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka jana.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki Poghisio alisuta vikali hatua hiyo akisema ni mapema mno kwa viongozi kuzungumzia siasa za uchaguzi mkuu ujao wakati wanafaa kuwa wakiwahudumia wananchi akisema kwamba huenda hatua hii ikaanza kuleta migawanyiko miongoni mwa wakazi.
Aidha Poghisio alielezea masikitiko yake kwamba ni viongozi wa kaunti ya pokot magharibi pekee wanaojihusisha na siasa za uchaguzi huku maeneo mengine yakijihusisha na maendeleo kwa wananchi.
“Inasikitisha kwamba viongozi katika kaunti hii wameanza kuendeleza siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 hali ni miezi michache tu baada ya taifa kukamilisha uchaguzi mkuu wa agosti mwaka jana. Hawa viongozi wanapasa kufahamu kwamba hatua hii itapelekea migawanyiko ya mapema miongoni mwa wananchi kwa mirengo ya kisiasa.” Alisema Poghisio.
Wakati uo huo Poghisio alidai kwamba huenda hatua ya chama cha KUP kujiondoa katika chama cha muungano wa azimio la umoja one Kenya ililenga kupisha nafasi ya chama hicho kujiunga na serikali ya Kenya kwanza baada ya azimio kufeli katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
“Ninavyoona chama cha KUP kilijiondoa kutoka muungano wa Azimio kwa lengo la kujiunga na serikali ya Kenya kwanza baada ya kuona kwamba muungano wa azimio umeshindwa katika uchaguzi mkuu. Na hilo si vibaya kwa sababu hakuna mtu anayependa kuwa upinzani. Kila mtu anapenda kujihusisha na serikal iliyo mamlakani.” Alisema.