VIONGOZI MBALIMBALI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WANAZIDI KUMLAUMU RAIS UHURU KENYATA


Hatua ya rais Uhuru kenyatta kutangaza wazi kumuunga mkono kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti imeendelea kuibua hisia miongoni mwa viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi hasa wanaoegemea mrengo wa naibu rais William Ruto.
Wa hivi punde kutolea hisia hatua hiyo ya rais Kenyatta ni aliyekuwa katibu katika wizara ya michezo na toradhi za kitaifa Simon Kachapin ambaye amesema kuwa huenda yote ambayo rais Kenyatta ametekeleza katika kipindi chake cha uongozi yakasahaulika iwapo hatakuwa makini kuhusu swala la uridhi wake.
Kachapin ambaye ametangaza nia ya kugombea tena kiti cha ugavana wa kaunti hii amesema kuwa Kenya ni taifa la demokrasia hivyo wakenya wanapasa kupewa fursa ya kujichagulia viongozi wao, kauli iliyosisitizwa na mbunge wa kapenguria samwel Moroto ambaye aidha amesema kuwa huenda washauri wa rais wanampotosha.
Kwa upande wake mbunge wa Sigor Peter Lochakapong amemtaka rais Kenyatta kuwa na heshima kwa naibu wake ikizingatiwa pale walipotoka naye huku pia akilaumu mwafaka baina ya rais na kinara wa ODM Raila odinga kuwa uliokusudiwa kumsaidia Raila kuwa rais wa tano wa taifa hili.