VIONGOZI KUTOKA KERIO VALLEY WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KUKABILI VISA VYA UVAMIZI.

Na Benson Aswani
Viongozi kutoka kaunti ambazo zimekuwa zikishuhudia wizi wa mifugo hasa eneo la Kerio valley wamehimizwa kuja pamoja na kupata suluhu ya kudumu.
Gavana wa kaunti ya Elgeyo marakwet Alex Tolgos amesema majibizano miongoni mwa viongozi hao kamwe hayatasaidia kuzima uovu huo ambao umegharimu maisha ya wakazi wengi huku wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.
Wito wake Tolgos unajiri siku moja tu baada ya mwakilishi wa kike kaunti hiyo Jane Chebaibai kutaka serikali kuajiri vijana kutoka eneo hili na kuwapa mafunzo ya kuhudumu kama askari wa akiba NPR ili kusaidia katika kukabili visa hivyo vya wizi wa mifugo kwani ndio wanaofahamu maeneo haya vyema.