VIONGOZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUENDELEZA KAMPEINI ZA AMANI

Viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuendeleza kampeni zao kwa heshima hasa wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Ni wito wake gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ambaye amesema kuwa viongozi wa kisiasa wanapaswa kuhakikisha wanatoa kipau kwa wakenya na taifa kwa jumla licha ya tofauti zao za vyama.
Aidha Lonyangapuo amewataka wakazi wa kaunti hii kuhakikisha wanafanya uamuzi wa busara katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwachagua viongozi wasio na ubinafsi.
Wakati uo huo Lonyangapuo amedai hatua yake ya kubuni chama kipya cha KUP ilichochewa na anachodai kufurushwa katika chama cha KANU licha ya kuwa mwanachama wa kwanza wa chama hicho kaunti hii ambapo kupitia kwake viongozi wengine walijiunga nacho.