VIONGOZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATAKA MKEWE MAREHENI MWAKILISHI WADI JOHNSTONE LOKATO KUMRIDHI KUONGOZA ENEO LA LELAN


Siasa za urithi wa mwakilishi wadi ya Lelan eneo la pokot kusini katika kaunti hii ya Poko magharibi Johnson Lokato ambaye aliaga dunia zimesheheni mazishi yake ambayo yameandaliwa hiyo jana.
Baadhi ya viongozi ambao walihudhuria hafla hiyo wakiongozwa na mbunge wa pokot kusini David Pkosing wamependekeza mmoja wa familia ya mwenda zake kuteuliwa katika bunge la kaunti hii kama heshima kwa marehemu Lokato kwa juhudi zake kuwahudumia wakazi wa wadi ya Lelan.
Ni ombi ambalo liliridhiwa na Uongozi wa chama cha UDA ambao umeahidi kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa familia ya mwenda zake inawakilishwa ili kujaza pengo ambalo ameliacha.
Simon Kachapin ni mgombea ugavana kupitia chama cha UDA.