VIONGOZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAONYWA DHIDI YA KUINGIZA SIASA SHULENI.


Wito umetolewa kwa viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kukoma kutumia raslimali za shule kuendeleza shughuli zao za kisiasa.
Akirejelea hafla iliyoandaliwa katika shule ya upili ya Kiwawa ya kuzindua chama cha UDA katika kaunti hii hafla iliyoongozwa na mbunge wa Kacheliba Mark Lumnokol , seneta Samwel Poghisio ameshutumu hatua hiyo akisema wanasiasa wanastahili kujitenga na raslimali za shule kwani si za mtu binafsi.
Poghisio ametoa wito kwa wadau katika sekta ya elimu kaunti hii ya Pokot magharibi ikiwemo wizara ya elimu, tume ya huduma kwa walimu TSC vyama vya walimu na wadau wengine kuingilia kati na kukomesha hulka hiyo.
Wakati uo huo Poghisio ameonya wanasiasa dhidi ya kuingiza siasa katika maswala ya uhamisho wa walimu kutoka shule moja hadi nyingine akidai wengi wanachochea uhamisho huo kutokana na tofauti baina yao na baadhi ya wakuu hao.