VIONGOZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAOMBOLEZA KIFO CHA ALIYEKUWA MWAKILISHI WADI YA KASEI.
Viongozi mbali mbali katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kutoa rambi rambi zao kufuatia kifo cha aliyekuwa mwakilishi wadi ya kasei kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2017 Samson Long’arkaye.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi ya Swam Robert Komole, viongozi hao wamemtaja mwenda zake kuwa kiongozi aliyekuwa mnyenyekevu, mtulivu na aliyeshirikiana vyema na viongozi wenzake.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwakilishi wadi ya Kapchok Peter Lokor ambaye pia amemwomboleza mwenda zake.
Marehemu alizikwa jumatano nyumbani kwake kamketo katika wadi ya kasei kaunti hii ya pokot magharibi.