VIONGOZI KAUNTI YA BARINGO WATAKA SWALA LA USALAMA KUANGAZIWA KWA DHARURA.


Serikali imetakiwa kuangazia kwa dharura tatizo la ukosefu wa usalama ambalo limeendelea kushuhudiwa kwenye baadhi ya maeneo ya kaunti ya Baringo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la viongozi wa kidini askofu Musa Kamuren, viongozi mbali mbali kaunti ya Baringo wameitaka serikali kuwatuma maafisa zaidi wa usalama kushika doria kwenye maeneo athirika ili kuwezesha wenyeji kurejea kwenye makazi yao.
Askofu Kamuren amesema kuwa kando na kaunti ya Baringo maeneo mengine nchini kama vile kaunti ya Lamu yameendelea kukabiliwa na tatizo la ukosefu wa usalama.
Aidha mwakilishi wa kike katika kaunti ya Baringo Gladwel Cheruiyot ameelezaa kusikitishwa na hali hiyo kwenye maeneo ya Baringo kaskazini na kusini ambako watoto na wanawake wanahangaika barabarani wakikimbilia usalama wao.