VIONGOZI KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUINUSURU HOSPITALI YA KAPENGURIA

Uongozi wa kaunti hii ya Pokot magharibi umeendelea kusutwa vikali kutokana na huduma duni katika hospitali ya Kapenguria uhaba wa vifaa muhimu ukitajwa kuwa chanzo cha masaibu ya wagonjwa.
Changamoto za ukosefu wa dawa katika hospitali ya kapenguria imesababisha wagonjwa kuteseka kwa muda bila huduma nzuri ya matibabu, chakula na maswala mengine.
Haya ni malalamishi ya wagonjwa katika hospitali hiyo.
Wamerai usimamizi wa hospitali hiyo kuchukua hatua haraka ili kushughulikia uhaba wa dawa na chakula kwa wagonjwa kwani wamehangaika kwa muda kutokana na huduma duni katika hospitali hiyo.
Wamesema licha ya kuwa wanalipa fedha za huduma katika hospitali hiyo hawajakuwa wakipokea huduma zinazostahili kutokana na uhaba wa vifaa muhimu.