VIONGOZI KAKAMEGA WAKASHIFU HOSPITALI YA BUTERE KWA UTEPETEVU


Viongozi wa kisiasa wakiwemo wawakilishi wadi kutoka eneobunge la Butere kauti ya KaKamega walitembelea hospitali ya Butere level 4 na kulaani kitendo ambacho mgonjwa alifariki na kusalia kwenye wadi kwa siku tatu akiwa na wagonjwa wengine kabla ya mwili wake kuondolewa
Viongozi hao wakiongozwa na mwakilishi wa Wadi ya Marama kusini Wilis Okuka Charles Nandwa wa Marama Kaskazini mwakilishi mteule kwenye kaunti ya Kakamega Christine Ogoma na Abel Nanjendo Bushuru wamesikitika na hali hiyo wakishtumu vikali usimamizi wa hospitali hiyo
Kutokana na sekta ya afya ambayo iligatuliwa na kuwepo na ukosefu wa vifaa vya matibabu na madawa na hata baadhi ya vitanda katika hospitali hii kukosa blanketi viongozi hao wamekashifu wizara ya afya na wizara ya fedha kuchangia masaibu ambayo yanashuhudiwa kwenye hospitali ya kaunti ya kakamega.
Wawakilishi wanne hao wamehoji kuwa watapeleka mswada kwenye bunge la kaunti hiyo kujadili utepetevu wa sekta ya afya kwenye hospitali na kuhakikishia wenyeji kuwa hali hiyo itatuliwa.