VIONGOZI ENEOBUNGE LA KACHELIBA WAMEWAHIMIZA WAKAAZI KUKUMBATIA AMANI MSIMU HUU WA SIASA.


Na Benson Aswani
Wakazi wa eneo la Kacheliba katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuishi kwa amani na utangamano na kutokubali kugawanywa kwa misingi ya kisiasa hasa wakati huu ambapo siasa za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao zimeendelea kushika kasi.
Mbunge wa eneo hilo Mark Lumnokol aidha amewataka vijana kutokubali kutumika na baadhi ya wanasiasa kuzua vurugu katika mikutano ya wapinzani wao kwa manufaa yao ya kisiasa na badala yake kusikiliza kila kiongozi anayezuru eneo hilo kuuza sera zake kwani mwishowe ni wao watafanya uamuzi wa kiongozi wanayemtaka.
Wakati uo huo Lumnokol ambaye pia ni mwandani wa naibu rais William Ruto ameendelea kumpigia debe Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao huku akipuuzilia mbali shinikizo za baadhi ya viongozi wa kisiasa kaunti hii za kuwataka wakazi kumuunga mkono kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.